Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya StatOil,
BG Tanzania, Exxon Mobil na Orphir Energy. Katikati ni Rais na Meneja Mkuu wa Kampuni ya BG Kanda ya Afrika Mashariki
Bw. Derek Hudson.
Rais na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Exxon Mobil Bw. Rolf Michael de Jong kwa niaba ya washirika wa
makampuni yanayofanya maandalizi
ya utekelezaji wa Mradi huo wa gesi iliyosindikwa (LNG) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa
kikao hicho.
Mkuu wa Mashauriano wa Kampuni ya StatOil Tanzania
Bw. Ole- Johan Lydersen wa kwanza mwishoni akiongea jambo wakati wa kikao
hicho.
Afisa Mipango Miji Bw. Daniel Nguno kutoka Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiongea jambo wakati wa kikao hicho
cha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa LNG.
======== ====== =======
Tufanyekazi, Watanzania wana matarajio makubwa na
gesi –Muhongo
Na
Asteria Muhozya, Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Watanzania wana
matarajio makubwa kutokana na kugunduliwa kwa hazina kubwa ya gesi katika maeneo
ya kina kirefu cha bahari.
Profesa
Muhongo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya
Statoil, BG Tanzania, Exxon mobil na Orphir Energy yanayofanya maandalizi ya utekelezaji
wa mradi wa gesi iliyosindikwa
(LNG).
Ameongeza
kuwa, Serikali inayo nia ya dhati katika kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha
kwamba uchumi wa gesi unakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote. Hivyo, wenye
jukumu la utekelezaji wametakiwa kutekeleza mipango mikakati yao kwa kuzingatia
muda husika, wakati huo huo wakifanyakazi kwa ushirikiano na mamlaka husika na
kwa uwazi.
“Wananchi
wana matarajio makubwa na gesi, msiiangushe Tanzania katika hili, hatutaki
kuonekana waongo, mkichelewa mnatupa wakati mgumu. Sisi sote tunatakiwa kuongea
lugha moja kwa wananchi. Tumejipanga vizuri tunachotaka ni kutekeleza mipango
yetu”. Amesema Profesa Muhongo.
Katika
hatua nyingine, Waziri Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, wamesisitiza
kuwa makampuni hayo, yanapaswa kuhakikisha
kwamba mipango yao ya utekelezaji wa
mradi huo inapaswa kwenda sambamba na matakwa ya Sera ya
Gesi Asilia.
Katika
kikao
hicho, makampuni hayo washirika yamewasilisha taarifa ya hatua
waliyofikia katika maandalizi ya utekelezaji wa mpango kazi wa
mradi huo na kueleza hatua mbalimbali
ambazo zimefikiwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili utekelezaji wa mradi
ufanyike kama ulivyopangwa.
Aidha,
katika taarifa hiyo wameainisha hatua mbalimbali ambazo watatekeleza katika
maeneo ambayo gesi imegunduliwa vikiwemo vyanzo vya Zafarani, Lavani na
Tangawizi katika kitalu namba 2 kilichopo mashariki mwa Mkoa wa Lindi.
Comments