NSSF YAENDESHA KAMBI ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KANDA YA ZIWA


Shirika la  Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendesha  kambi za upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma  kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;

Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.
NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
 Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya  virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.
Wakazi wa Mkoa wa Mara wakisubiri kumuona daktari kupata ushauri.
 Daktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lucy Simbila (kulia), akimpima shinikizo la damu mmoja  ya  watu waliojitokeza  kupima afya mkoani Mara juzi, katika kambi ya Upimaji Afya Bure inayoendeshwa na NSSF katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Madaktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakimpa ushauri mmoja wa watu waliofika kupima afya.
Madaktari na Maofisa wa NSSF walioendesha kambi ya upimaji wa afya mkoani mara wakiwa katika picha ya pamoja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

CHAKUHAWATA WANENA MAKUBWA--