BONDIA MAARUFU WA KIKE BINTOU SCHMILL ULINGONI 26.9.2014 FRANFURT,UJERUMANI

Prof.Female boxer Bintou Schmill based in Germany
Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill aka “The Voice” anatarajiwa kupanda ulingoni tarehe 26 September 2014, atapambana na bondia  Mirjana Vujickatika ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied, Mjini Frankfurt ujerumani.
Bondia Bintou Yawa Schmill aka “The Voice” mzaliwa wa Togo ambaye anapigia uzito wa Welterweight -64 Kg, urefu mita 1.71  historia yake hapo mwanzo alikuwa bondia wa ngumi za ridhaa kwa muda miaka mitano,kuanzia mwaka 2007 alianza kuingia katika ngumu za kulipwa (professional boxer) amepigana (fights) 8 kashinda 7(wins) kashinda kwa
K.O.s 7.
Bondia Bintou Yawa Schmill ni juzi tu katimiza umri wa miaka 30,mwanafunzi wa chuo kikuu cha Bremen na ndiye aliyelipamba jarida la maarufu la warembo “Penthouse”,bondia huyo wa kike anayeiliwakilisha bara Afrika Ughaibuni mara nyingi amefananishwa
na SIMBA (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou “The Voice” Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...