Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kushoto akipongezwa na mmoja kati ya wapiga kura wa kijiji cha Kiwere |
Mfanyabiashara wa nyama choma Kiwere kulia akimweleza mbunge Mgimwa jambo baada ya kutembelea vijana na wananchi wanaojishughulisha na biashara eneo la magenge ya Kiwere |
wanakikundi cha uoteshaji miti Kiwere wakimweleza mikakati yao mbunge Mgimwa katikati |
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akipita kwa shida katika vichaka baada ya kwenda kuwatembelea wapiga kura wake kijiji cha Kiwere |
Kama anazungumza vile "lazima nimefike kuona kazi za wapiga kura wangu " |
Mbunge wa Kalenga Bw Mgimwa katikati akiruka maji ili kwenda kuona mto ambao unatumika kuwapa huduma ya maji wakazi wa Kiwere |
Wanachama wa VICOBA Kiwere wakiimba shairi mbele ya mbunge Mgimwa |
Diwani wa kata ya Kiwere Pachal Mwano akizungumza kabla ya kumpongeza mbunge Mgimwa kwa kazi nzuri |
Mbunge Mgimwa akizungumza na wanachama wa Vicoba Kiwere |
Na Matukiodaima.co.tz
WANACHAMA wa vikundi vya VICOBA kata ya Kiwele katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa wapongeza jitihada za mbunge wao Godfrey Mgimwa kwa kuwachangia kiasi cha Tsh milioni 3 ili kukuza mfuko wa vikundi hivyo kata ya Kiwele.
Akitoa pongezi hizo jana kwa niaba ya wanachama wa VICOBA kata ya Kiwele diwani wa kata hiyo Paschal Mwano alisema kuwa kata hiyo ni miongoni mwa kata zenye ndoto kubwa ya kuanzisha benki ya wananchi wa kata ya Kiwele hivyo kutokana na jitihada mbali mbali mbali zinazofanywa na wananchi hao kwa kuungana katika vikundi hivyo ipo siku watafikia hatua ya kuwa na benki
Kwani alisema kuwa fedha hizo kiasi cha Tsh milioni 3 zilizotolewa na mbunge huyo zitasaidia kukuza mtaji wa vikundi hivyo 22 zilivyopo katika kata hiyo yenye vijiji vitano kikiwemo cha Kiwere , Mgera, Mfyome ,kitapilimwa na Itagutwa .
Alisema kuwa vikundi hivyo hivyo vina jumla ya wanachama 464 wakiwemo wanawake 386 na wanaume 78 na hadi sasa wana jumla ya Tsh 33835000 na kuwa kutokana na na faida mbali mbali wanazozipata katika vikundi hivyo wanachama wameweza kuanzisha miradi mbali mbali ikiwemo ya ufugaji kuku ,bata nyuki na miradi mingine mingi ambayo imewasaidia kukuza uchumi wa mwanachama mmoja mmoja.
Mbali ya kujiwezesha kwa mikopo bado wanahitaji kusaidiwa mitaji zaidi ili kuanzisha miradi ya ufugaji ng'ombe wa maziwa na kuku wa nyama na mayai kama njia ya kuongeza miradi zaidi.
Kwa upande wake mbunge Mgimwa pamoja na kuwapongeza kwa kuanzisha vikundi hivyo 22 vya vicoba bado alisema kuwa kasi kubwa ya wananchi kuendelea kujiunga na vikundi hivyo vya Vicoba ndio itakayopelekea jimbo la Kalenga kuja kuwa na benki ya wananchi wa Kalenga jambo ambalo linawezekana.
" Nawapongeza sana wananchi wa kata ya Kiwere kwa kuendelea kujiunga na Vicoba kwani naamini njia pekee ya kujikomboa kiuchumi ni pamoja na hii ya kujiunga pamoja ......kwa hatua ambayo mmefikia tunaweza kufanya jambo kubwa zaidi ya hili mimi leo nitawachangia kiasi cha Tsh milioni 3 ili kukuza mtaji zaidi " alisema mbunge Mgimwa
Aidha alisema kuwa tatizo kubwa katika vikundi hivyo vya kifedha ni pale ambapo wanachama wanakopa na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati na hivyo kukwamisha wanachama wengine kukopa .
Kuwa iwapo wanachama watashindwa kurejesha mikopo kikundi ama vikundi hivyo havitaendelea na badala yake vitakufa mapema hivyo kuwataka wakopaji kulipa mikopo kwa wakati kama njia ya kuviendeleza vikundi hivyo.
Mbunge Mgimwa alisema kuwa kitaalum yenye ni mtaalam wa fedha hivyo kwa kupitia uwezo wake ndio sababu ya bunge kumteua kuwa mjumbe wa kamati ya bunge ya bajeti ya serikali na wana kalenga wazidi kujivunia kumpata mbunge mwenye ndoto ya kuona jimbo hilo linakuwa na benki ya wananchi wa Kalenga jambo ambalo linawezekana kufanyika.
Comments