Ilikuwa
ni Moja ya Safari ambazo zilikuwa na Mafanikio Makubwa ambapo Tone
Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya Yetu Blog tuliamua kuanza
Rasmi kuvitangaza vivutio vya kitalii ambavyo tunaamini vimesahaurika
kwa njia moja au yengine, katika Safari yetu ya kuvitangaza vivutio
hivyo tumeanza moja kwa moja na Mkoa wa Mbeya.
Kwanza kabisa tulifika katika Kijungu na Kujionea mengi.. Kama ulikosa kuona juu ya kijungu Bofya hapa MBEYA YETU ILIPOTEMBELEA KIJUNGU
Leo
katika mwendelezo wa vivutio hivyo vya Utalii katika Mkoa wa Mbeya
tutakiangazia kivutio kimoja wapo ambacho ni Maporomoko ya Kaparogwe,
Maporomoko haya ni moja ya Kivutio kikubwa cha Utalii Nchini Tanzania
ambacho kinavutia sana.
Maporomoko
haya ambayo yapo Kilometa 11 kutoka Ushirika Tukuyu sehemu ambayo kuna
barabara nzuri na Gari la aina yoyote inaweza kufika katika kivutio
hicho.
Kikosi
kazi cha Mbeya yetu tulifika eneo Hilo na kujionea wenyewe eneo hilo na
kujionea Maliasili hii na eneo ambalo kwa hakika linahitajika
kusapotiwa na kulitangaza ili Dunia ipate fahamu kuwa kuna eneo kama
hilo na wanahitaji kufika na Kutembelea.
Hivi ndivyo Safari yetu ilivyokuwa.. Fuatilia hapa
Hii ni njia yakuelekea Maporomoko ya Kaporogwe
Utalii wa ndani baadhi ya watu wanaelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe
Huu ni upande wa kuingilia kwa mbali ndivyo maporomoko yanavyo onekana
Kama kawaida unapotembelea maeneo kama haya lazima upate ukodaki wa kumbukumbu hapa kila mmoja akichukua matukio
Kwa
hakika Joseph Mwaisango Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu akiwa mwenye
furaha alipofika katika maporomoko haya ya kaporogwe mara baada ya
kujionea yeye mwenyewe. Hapa ni eneo la Ndani kabisa ya Maporomoko hayo.
Hili ni Moja ya eneo la Mapumziko, watu wanaofika huja hapa na kukaa kisha kutazama uzuri wa Maporomoko ya Kaporogwe Maji yakiwa yanashuka kwa kasi katika maporomoko ya Kaporogwe
Kwa Jirani kabisa Maji yanavyomwagika katika Maporomoko ya kaporogwe
Unaweza ukaona maajabu sana lakini hii ndio njia ya kuingilia maporomoko ya kaporogwe
Head
of Group Research and Product Development wa Tone Multimedia Group
ambao ni Wamiliki wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje akiwa chini
kabisa ya Maporomoko ya Kaporogwe kujionea jinsi maji yanavyo mwagika,
katika eneo hili la chini kuna hali ya unyevu vyavu na baridi ya aina
yake ambayo haiumizi lakini inayohamasisha kuendelea kuwepo katika eneo
hilo muda wote.
Hii ni Barabara inayotokea eneo Linaitwa Kissa kuelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa Kwanza kulia akiwa na wenyeji wanaokaa maeneo ya Maporomoko ya Kaporogwe.
Wa kwanza kulia ni Fredy Anthony Njeje akiwa pamoja na wakazi wanaoishi maeneo ya Kaporogwe Hii ni Barabara nzuri ya Kuelekea katika maporomoko ya kaporogwe.
Imeandaliwa na Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wake wa Mbeya yetu Blog ambao upo ndani ya Blogs za Mikoa.
Je
unapenda kutoa maoni au kuungana nasi katika kampeni hii Piga simu ama
tuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia +255 765056399 au +255 754374408.
Comments