Pichani ni Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi elfu moja, kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Noti hizo zitaanza kutumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, kuanzia tarehe Mosi Februari, 2025. Kwa mujibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emanuel Tutuba, Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu. Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini. “Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa z...
Comments