From Town:
From Kimara: Sam Nujoma - Nelson Mandela (upper floor): FYI: Images grabbed from the simulation as presented Kazi kwenu... |
Soma hii:
‘Flyover’ Ubungo
Akizungumzia barabara hiyo ya juu ya Ubungo, Mkuu Idara ya Usanifu na Viwango wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Ebenezer Mollel alisema katika eneo la Ubungo kutakuwa na barabara za ngazi tatu ambazo zitakuwa katika mifumo isiyowezesha msongamano wa magari.
Mollel alisema barabara za mabasi yaendayo haraka (BRT) itaendelea kufanya kazi kama kawaida ikiongozwa na taa, huku magari yanayotoka barabara ya Sam Nujoma na Mandela, mfano Buguruni - Mwenge au Mwenge - Buguruni yatakuwa yakipita juu.
“Katika barabara ya kwanza magari kutoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Buguruni (Mandela) na Kimara (Morogoro) kwenda Mwenge (Sam Nujoma) yataongozwa na taa. Magari yanayotoka Buguruni kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatafuata mfumo wa taa,” alisema Mollel.
“Katika barabara ya pili magari yanayotoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatatakiwa kuongozwa na taa na hii ‘Flyover Interchange’ haitakuwa na msongamano kwani kila gari litakuwa na njia yake na hakutakuwa na msongamano wowote.”
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa
barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
PICHA
NAMBA 2
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa
barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za mikataba
mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa
maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la
ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi
ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji
saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.
Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), leo umetiliana saini na kampuni ya M/S China
Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika
makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.
Mkataba
huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara
moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza
mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini
TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4
zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi
mwaka huu.
“Hakikisheni
mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari
kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi
walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng.
Mfugale.
Ujenzi
wa Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo
Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1
“Zaidi
ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara za
morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano
katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es
salaam hivyo ufanisi wa mradi huo
utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji
wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia
Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi
hiyo kwa wakati.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Comments