EWURA YACHANGIA MADAWATI KWA WANAFUNZI 150 SHULE YA MSINGI KILOLENI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, leo, 11/10/24, imekabidhi madawati 50 yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi 150 wa shule ya msingi Kiloleni yenye usajili P1903011 iliyopo manispaa ya Tabora.

Mkuu wa Shule hiyo, Rajabu Kiama ameishukuru EWURA kwa kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule hiyo.

“Uongozi wa shule unatoa shukrani kwa EWURA kuunga mkono juhudi za kutatua changamoto hii ya upungufu wa madawati kwa wanafunzi, ambayo yatawapa fursa wanafunzi 150 kukalia madawati”, alisema

Ofisa Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Getrude Mbiling’i, akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Mamlaka, amewaasa wanafunzi wa shule hiyo kutunza samani walizopatiwa.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme, gesi ya kupikia na utaratibu wa EWURA wa kushughulikia malalamiko yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa katika sekta za nishati na maji.

Kiloleni ni miongoni mwa shule kongwe iliyopo Kata ya Mapambano, Halmashauri ya Tabora na ilianzishwa mwaka 1970. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1050; wavulana 520 na wasichana 530 na jumla ya walimu 13.

Mkuu wa Shule ya Msingi Kiloleni, Rajabu Kiama (kulia) akiishukuru EWURA kwa kuwezesha ununuzi wa madawati yaliyokabidhiwa shuleni hapo na Ofisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Bi Getrude Mbiling’i (wa pili kushoto) Oktoba 11, 2024. Anayeshudia kushoto ni mtumishi wa EWURA wa Kanda hiyo, Elly Mmbaga.

 Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiloleni ya mkoani Tabora, wakiwa na machapisho mbalimbali ya EWURA baada ya kupata elimu kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme, gesi ya kupikia na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko EWURA kuhusu huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka kutoka kwa maofisa wa EWURA wa Kanda ya Magharibi,.

   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiloleni ya Tabora, wakiwa wameketi katika madawati yaliyokabidhiwa na EWURA Kanda ya Magharibi, shuleni hapo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO

NDOGO WA MUME WANGU ALIKUWA EX WANGU