UVCCM YATEMBEA KWA MIGUU IKIFUATA NYAYO ZA BABA WA TAIFA KUTOKA BUTIAMA HADI MWANZA

Vijana 2,100 wakiwemo 32 wa kutoka Musoma Vijijini, walianza matembezi ya miguu kutokea Butiama hadi Mwanza siku ya Jumatano, 9.10.2024.


Matembezi haya yanafuata nyayo za matembezi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyafanya Mwaka 1967 akiunga mkono Azimio la Arusha lililozaliwa mwaka huo (1967)

Vilevile, matembezi haya ni sehemu ya sherehe za kilele cha ukimbizaji Mwenge wa Uhuru zitakazohitimishwa Jijini Mwanza tarehe 14.10.2024

CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa inaelezea baadhi ya matukio ya tarehe 9.10.2024 ya Kijijini Butiama - tafadhali isikilize.

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO

NDOGO WA MUME WANGU ALIKUWA EX WANGU