AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO


 Sure Boy, Andabwile ‘watemwa’ Yanga ikiifuata MC Alger


BENCHI la Ufundi la Yanga chini ya Kocha Mkuu Sead Ramovic, limetangaza majina ya ‘askari 24 wa Jeshi la Wananchi’ hao wanaokwea pipa leo alasiri ya leo Jumanne Desemba 3, kwenda Algiers, nchini Algeria, kuwavaa Mouloudia Club d’alger ‘MC Alger,’ huku Salum Aboubakar ‘Sure Boy na Aziz Andabwile wakiachwa.


Yanga watakuwa wageni wa MC Alger Jumamosi ya Desemba 7, katika mechi ya pili ya Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2024/25), wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Hilal ya Sudan, huku Waalgeria hao wakitoka kugawana pointi na TP Mazembe katika mechi ya kwanza.


Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga, kikosi chao kinajumuisha wachezaji 24, wakiwemo nyota wao kadhaa waliokuwa majeruhi na waliokuwa wakitumikia adhabu zilizowakosesha mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa, Lindi.


Katika orodha ya nyota wanaokwea pipa alasiri hii ya leo, Yanga itaongozwa na walinda mlango, ambao ni Djigui Diarra, Aboubakar Khomeiny na Abutwalib Mshery, huku mabeki wakiwa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca,’ Yao Kouassi, Nickson Kibabage, Kibwana Shomari na Chadrack Boka.


Msafara huo unajumuisha viungo Khalid Aucho, Mudathir Yahaya Abbas, Jonas Mkude, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Dennis Nkane, Farid Mussa, Shekhan Ibrahim Khamis, Pacome Zouzoua, Clatous Chama na Stephanie Aziz Ki, huku washambuliaji wakiwa ni Jean Othos Baleke, Kennedy Musonda, Clement Mzize na Prince Dube.


Licha ya kuelezwa kuwa amepona majeraha yaliyomuweka nje ya kikosi kwa muda mfupi, nyota Aziz Andambwile ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga walioachwa katika safari hiyo, kama ilivyo kwa kiungo fundi Salum Aboubakar ‘Sure Boy.’


Yanga wanahitaji ushindi kwa udi na uvumba ili kuweka hai matumaini yao kufanya vema na kupigania nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo, sawa na ilivyo kwa wenyeji wao hao ambao watakuwa wakipambania matokeo chanya ili kujiweka mahali salama kwenye msimamo wa Kundi A.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

AHMED ALLY KULIPA BIL. 10 KWA KUIKASHIFU YANGA