CHATANDA AMPONGEZA FATMA REMBO KWA KUIWEZESHA UWT MKOA WA IRINGA MIL. 54

MWENYEKITI wa jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania ambae pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mary Chatanda amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na mjumbe wa baraza kuu la CCM Taifa ambae pia ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT Taifa Fatma Rembo kwa kutoa sh.54 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT mkoa wa Iringa.

Fatma Rembo aliikabidhi UWT mkoa wa Iringa sh.54 millioni ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo baada ya kuona inasuasua kukamilika ujenzi wake wakiwemo wabunge wa viti maalum mkoa pamoja na wadau wengine ambao walichangia ujenzi huo.

‘’Nichukue nafasi kukupongeza mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la UWT Taifa ndugu Fatma Rembo kwa kukamilisha jingo hili hadi kufikia hapa.Hakika unaitendea nafasi yako,kwa kuweka alama kwenye mkoa wako wa Iringa;

Nimesikia kwenye taarifa ya ujenzi,wamesema umetumia sh. 54 millioni,siyo jambo dogo,hongera sana kwa kuitendea haki nafasi yao ya ujumbe wa kamati ya utekelezaji baraza kuu la UWT Taifa”Amesema.

Amesema chama cha Mapinduzi ccm kinachoongozwa na Mwenyekiti wa ccm Taifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan walitoa maelekezo ndani ya halmashauri kuu Taifa kwamba ni vizuri chama na jumuiya zake zinajenga nyumba kwa ajili ya watumishi ili wanapopata uhamisho kwenda eneo jingine,wapate makazi ya kuishi.

“Hivyo ninapenda kutoa agizo nchi nzima kwa mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya wahakikishe wanakamilisha.

Katika hatua nyingine,Chatanda ameweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT wilaya ya Iringa mjini huku akihimiza nyumba hiyo ikamilike kwa haraka ili iweze kuzinduliwa februari 2025 na kuanza kutumika.

Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda leo disemba 30 anahitimisha ziara yake ya siku nne mkoani Iringa.Ziara hiyo ilianza Novemba 27 ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wa mkoa huo,kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha tarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI