Februari 20, 2025 nikiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo tumefanya ziara katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro, kushuhudia mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho K4.


Nimeupongeza uongozi wa kiwanda kwa mradi huo wenye tija na maslahi katika kukuza uchumi wa taifa, kuboresha maisha ya watu na kukabili changamoto ya uhaba wa sukari nchini.

Dhimba ya ziara yetu ni kujionea uwekezaji wa kimkakati katika miradi mikubwa, inayolenga kuiwezesha nchi kutimiza lengo lake la kujitosheleza kwa uzalishaji wa sukari na kutengeneza fursa ya soko kwa wakulima wa miwa kwenye Bonde la Kilombero.

Naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rahisi ya biashara, pia naupongeza uongozi wa Kiwanda cha Kilombero chini ya Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Ami Mpungwe kwa kusimamia mradi huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 5 YA KILA MWANANDOA KUFAHAMU