WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE AITAKA CMA KUWA TAASISI YA KIMKAKATI KUTATUA MIGOGORO YA KAZI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameitaka   Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kuwaTaasisi ya kimkakati katika utatuzi wa migogoro ya kikazi nchini ikiwa na lengo la kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kuhakikisha mahala pa kazi panakuwa na amani ili kuwafanya  wafanyakazi na waajiri watumie muda mwingi kufanya uzalishaji Wenye Tija.


Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Utendaji Kazi na mafunzo kwa watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania bara, kilichofanyika Leo tarehe 19 Februari, 2025 Mkoani Morogoro.u


Aidha, Mhe. Kikwete ameitaka Tume hiyo kushughulikia migogoro kwa haraka, ufanisi na weledi ili kuweza kutimiza matarajio ya wadaawa na wadau ambao wengi wao ni wawekezaji, hivyo kusaidia kukuza Uchumi wa nchi.


"Serikali iliongeza bajeti ya Tume kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni mia tisa (900,000,000+) bila shaka mmeona ongezeko hilo limeleta mabadiliko siyo tu kwenye maslahi ya wafanyakazi lakini pia kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake ya msingi" amesema Mhe. Kikwete


Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose Mlyambina amewakumbusha wasuluhishi na waamuzi kutilia mkazo suala la matumizi ya mfumo wa kielekroniki na hususani kuangalia namna bora ya kupokea  vielelezo ili kuwasilisha jalada kamilifu pindi litakapoitishwa mahakamani.


Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla amemhakikishia Waziri   Kikwete kuwa Tume hiyo ya itaendelea kuwa Taasisi ya kimkakati katika kukuza uchumi nchini kwa kuimarisha utatuzi wa migogoro ya kikazi nchini ili kuweza  kuhakikisha mahala pa kazi panakuwa na amani na kuwafanya  wafanyakazi na waajiri watumie muda mwingi kufanya uzalishaji Wenye Tija.




 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 5 YA KILA MWANANDOA KUFAHAMU

SALMA KIKWETE, WAWATA WAMPAISHA PROF. NDAKIDEMI