CHATANDA AWATAKA WAJUMBE KUJIEPUSHA NA SUALA LA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

Wagombea 32 wa makundi manne kuingia katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Viti Maalumu Taifa kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi wa UWT utakaofanyika kesho Jumamosi klwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Agosti Mosi, 2025, kuhusu maandalizi ya mkutano huo utakaohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 1,100 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Ametaja makundi hayo kuwa ni; Wafanyakazi, NGO's, Wasomi wa vyuo vikuu na Watu wenye ulemavu ambapo kila kundi watakuwa wagombea 8 watakaopigiwa kura na wajumbe.

Amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na wajumbe kutoka mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Visiwani wameshawasili.

Aidha, Chatanda amekemea vikali kwa wajumbe wote watakaochagua wagombea ubunge kwa kutumia rushwa. Amewataka kuchagua wabunge wanaowapenda badala ya waliotoa rushwa.







 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MSIMAMIZI MKUU
 KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...