Wanafunzi na wananchi wengine wakipata elimu kuhusu Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA-CCC), walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Wananchi waliofika hapo waliambiwa kwamba mtumiaji wa huduma za Usafiri Ardhini ni abiria anayesafiri kwenye basi la masafa marefu, basi la mijini (daladala),Taxi, Taxi Mtandao, Pikipiki za magurudumu mawili au matatu, pamoja na treni za abiria.
Baraza hilo limeundwa kisheria ambapo walisema abiria awapo safarini ana haki zifuatazo; Usalama,kupata mahitaji muhimu, kupewa taarifa awapo safarini,kuchagua,kusikilizwa,kulipwa fidia, kusafirii katika mazingira salama, kuelimishwa na haki ya kugomea huduma au bidhaa zisizokidhi viwango.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miuji B, wakisikiliza maelezo
Comments