SIKU YA WACHAGA YAFANA SANA MJINI MOSHI
chagga day ilivyopambwa ndani ya zumbaland mjini moshi.
boda 2 boda wakiwajibika jukwani shoo ya chagga day moshi ndani ya zumbaland.
ommy dimpoz akiimba na washabiki chagga day moshi.
ommy dimpoz akimuimbisha mtoto shoo ya chagga day ndani ya zumbaland.
thecla mgaya 'aisha' wa mambo hayo alikuwemo ndani ay nyumba akifurahia chagga day pale zumbaland moshi.
baadhi ya wanamuziki wa serengeti band ya arusha kabla ya kutumbuiza tamasha la chagga day moshi ukumbi wa kisasa wa zumbaland.
mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.
Tamasha kubwa la kihistoria
lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika
kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi
tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na
kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na
familia zao.
Tamasha hilo lililotawaliwa na
shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika
kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na
kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake
Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari
Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua
cha Pepsi.
Comments