UTPC YAPINGA MAOMBI YA CHADEMA KUTAKA KUIHUSISHA IPC KTK UJENZI WA MNALA WA DAUDI MWANGOSI
Makamu mwenyekiti wa UTPC Bi Jane Mihanji akitoa tamko la UTPC dhidi ya Chadema kutaka kutumia kifo cha Mwangosi kisiasa
Rais wa UTPC Bw Keneth Simbaya kushoto akimpongeza makamu wake Bi Jane Mihanjo kwa tamko zuri alilolitoa
Akitoa
tamko kwa niaba ya bodi ya UTPC jana , Makamu wa Rais Jane Mihanji
wakati mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho
ya Katiba ya UTPC uliyofanyika Mjini Dodoma kwa muda wa siku mbili.
Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutumia vifo kama mtaji wa kisiasa. |
“..Sisi kama UTPC tunatoa
tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie kifo cha Daudi Mwangosi
katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na swala hilo au zoezi hilo la
kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa
kufanywa na chama hicho’Alisema Mihanji.
|
Alisema ujenzi wa mnara huo ambao
inatarijiwa kufanywa na chama sio kazi yao kwa ili wanatafuta umaharufu wa
kwenye majukwaa na kuwataka waache wakawaachia
wahusika wenyewe jumuhia za waandishi wa
habari ambao ndiyo wenye mamlaka na si vinginevyo.
|
Mihanji alisema kuwa, Mwangosi hakuwa
mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu katika tasnia ya habari “Kwani yeye
kufuatia mauaji yake hakuwa katika
harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo wenye
mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni wahusika ambao ni
wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.
|
“UTPC ndiyo wenye mamlaka ya
kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho kwahiyo ni vema swala hilo
waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo wahusika kwahiyo tunajua nini
tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwahiyo tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho
swala hilo liachwe na tuachiwe wenyewe”Alisema makamu wa rais huyo.
|
Mwangosi alikuwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Chanel ten Mkoani Iringa ambaye pia alikuwa
ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo (Iringa Press Club)
ambapo ameuawa mikononi mwa jeshi la polisi mnamo 2012.
Hata
hivyo hadi sasa bado suala la kifo cha Mwangosi limeendelea kupigwa
dana dana kutokana na kesi yake kutosikilizwa na hakuna mwandishi
aliyeitwa kutoa ushahidi wake juu ya mauwaji hayo .
Mwangosi
hakuuwawa kama mwanachama wa Chadema bali aliuwawa akiwa kazini
kutimiza wajibu wake wa kitaalum ya uandishi hivyo kwa kitendo cha
Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi huo itakuwa ni
kuvuruga mwenendo wa kesi na kupingana na msimamo wa awali ya IPC ,UTPC
na vyombo vingine kuhusu taarifa za awali ambazo jeshi la polisi
lilianza kutaka kupotosha kuwa eti alikuwa ni mwanachama wa Chadema
jambo ambalo si kweli.
Sikiliza VIDEO yake katika You tube ( andika Tamko la UTPC ) |
Comments