Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua nyumba hiyo ya zamani
iliyokuwa inatumiwa na Mfugaji Mihangwa, kabla ya kujenga nyumba ya
kisasa katika Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni. Singida.
Kinana
akiangalia mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza
mingine kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa. Mihangwa anasema aliamua
kuuza ng'ombe 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
Kinana akizindua nyumba Mfugaji huyo ya kisasa kabisa . Kulia ni Mfugaji Mihangwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (haonekani pichani) na wajumbe wengine wakitoka nje ya nyumba ya kisasa ya Mfugaji Mihangwa mara baada ya kuikagua,Bwan.;Mihangwa aliuza ng'ombe zake 200 na kubaki na ng'ombe 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa kama ionekanavyo pichani.
jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka kama lionekanavyo pichani
Kinana
akisaidia kumpatia tofali fundi wa jengo la maabara ya Shule ya
Sekondari Heka wakati wa ziara yake katika Jimbo ya Manyoni Mashariki.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligat
Kinana akilakiwa na mabango katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka wakati wa ziara yake wilayani Manyoni.
Nape
akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, ambapo
aliwaambia wananchi kuwapuuza wapinzani kwani hata wakifanya mkutano
hawasaidii wananchi katika masuala ya maendelo, bali wamebaki wakihubiri
suala ya Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtambulisha Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki,Kapt.John Chiligati kwa wananchi wa Kijiji cha Heka katika mkutano wa hadhara.Aidha Mh.Chiligati alielezea katika mkutano huo miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika eneo hilo la Heka.
Wanachama
wapya wakila kiapo ha utii cha CCM baada ya kujiunga na chama hicho
katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, Manyoni.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki mazoezi ya Wanafanzi walioko
kambini kwa ajili ya mashindano ya UMISSETA wilaya ya Manyoni jioni ya
leo mkoani Singida.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia kwenye mkutano wa
hadhara ambao pia ulihudhuriwa na Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika
Stendi ya Manyoni, willayani Manyoni, Singida leo. Nape amesema kitendo
cha vyama vya upinzani kuunda Ukawa umekirahisishia CCM kuvishambulia
vyama hivyo kwa pamoja badala ya kimoja kimoja.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatulia yaliyokuwa yakizungumzwa uwanjani hapo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara
katika Stendi ya Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba
tunaitaka, lakini isiwe ya mazingaombwe
ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho, tusing'oane meno kwa
ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi
kuwa ya maziwa" alisema Kinana akatika mkutano huo..
Mbunge
wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati akiwahutubi
wananchi wa mji wa Manyoni mapema leo kwenye stendi ya mabasi Manyoni.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
katika Stendi ya Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba
tunaitaka, lakini isiwe ya mazingaombwe
ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho, tusing'oane meno kwa
ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi
kuwa ya maziwa" alisema
Kinana akatika mkutano huo.Ndugu Kinana yupo mkoani humo kwa ziara ya
siku 8 akitokea mkoani Tabora ambako alikuwa na ziara ya siku 11.
Comments