Kiwanda cha Sukari cha Kagera tayari kilishaanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari Nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari Tanzania na Nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani hapo.
Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.
Mto wa Kagera ni kati ya mito inayounda mto wa Nile pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza. Inaanza Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela 400 km hadi kuingia ziwa la Victoria Nyanza.
Mto wa Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale inapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho wa njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza kama 40 km kaskazini za Bukoba. Jina la Mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.
Comments