Na Mwandishi Wetu- Arusha
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imedhamiria kufanya mabadiliko katika Sera zake mbalimbali ili kuweza
kuendana na wakati na kuwezesha kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa
huduma kwa watanzania.
Katika
kulifanikisha hilo Wizara imeamua kuipeleka Sera ya Taifa ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 kwa wadau ili iweze kutolewa maoni na
baadae kufanyiwa marekebisho kuiwezesha kuendana na wakati.
Akifungua
kikao kazi cha wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali kuijadili Sera
ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Arusha, Katibu Mkuu
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa maoni ya
wadau ni muhimu sana katika mchakato wa maboresho wa Sera hiyo.
Bibi.
Sihaba Nkinga ameleza kuwa Serikali imeamua kuwashirikisha wadau hao
kwani kwa asilimia kubwa ndio watekelezaji wa Sera hiyo katika majukumu
yao ya kila siku.
Ameongeza
kuwa Serikali inatambua mchango wa kazi zinazofanywa na Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini na zoezi hili la kuiboresha Sera hiyo
litaleta mageuzi makubwa katika Sekta.
Katibu
Mkuu Sihaba Nkinga amesisitiza kuwa upatikanaji wa Sera nzuri utasaidia
kupata Sheria nzuri na kukiwa na Sheria nzuri itasaidia utendaji mzuri
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
“Tuitumie fursa hii kujadiliana vizuri ili tupate Sera itakayopeleka Sekta yetu ya NGOs mbele” alisisitiza Bibi. Sihaba.
Kwa
upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Marcel
Katemba amewataka wadau kuzingatia kikao kazi hicho kwani ndio fursa ya
kutoa maoni yao ya kuiboresha Sekta ya Mashirika ya Yasiyo ya
Kiserikali nchini
Naye
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw.
Nicholous Zakaria ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na kuahidi
kuendelea kusimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuratibu
upatikanaji wa maoni kwa ajili ya maboresho ya Sera ya Mashirka Yasiyo
ya Kiserikali nchini.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha
kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Msajili
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Marcel Katemba akitoa ufafanuzi
kuhusu masuala mbalimbali ya kisera wakati wa ufunguzi wa kikao kazi
kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau wa NGOs kujadili
maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Nicholous
Zakaria akieleza kuhusu umuhimu wa Baraza katika kuratibu utendaji kazi
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini wakati wa ufunguzi wa kikao
kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili
maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada
mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha
kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Katibu
Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali nchini mara baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika
Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya
Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali watatu kulia waliokaa ni
Mkurugenzi na Masajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel
Katemba. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Comments