ASKOFU DKT. BAGONZA ATAKA MWENGE UWAMULIKE NA UWACHOME MAADUI WA MAENDELEO NCHINI


 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Karagwe Dk. Benson Bagonza ameutaka Mwenge wa Uhuru 2024 kuwamulika maadui wa maendeleo waliomo Nchini ikiwa ni katika dhana ya kuwafichua maadui wa maendeleo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Askofu Bagonza ametoa wito huo wakati alipopata nafasi ya kutoa salaam zake kwa Wananchi wa Wilaya ya Karagwe eneo la Kishao, wakati wa tukio la uzinduzi wa Mradi wa Barabara yenye ya lami Kishao - Lukajange yenye urefu wa Km 0.7 yenye thamani ya Shilingi Milioni 358.08 inayotekelezwa chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).


Katika salaam hizo Askofu Bagonza amewakumbusha Wananchi historia na dhana ya Mwenge wa Uhuru toka ulipopandishwa juu ya Mlima Kilimanjaro na Brigedia Alexander Donald Nyirenda mwaka 1961, ilikuwa ni kuwamulika maadui waliopo Nje na Ndani ya mipaka ya Nchi yetu.


 "Lakini kwa Sasa Maadui wa namna hiyo hawapo tena, bali wameibuka maadui wa ndani ya Nchi wapinga miradi ya maendeleo, hivyo Mwenge wa Uhuru uendelee kuwamulika na kuwafunua ili Wananchi waendelee kunufaika na miradi kama hii ya Maendeleo inayoletwa na Serikali."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI