ETOO ATAKA TANZANIA IWE NA TIMU NANE MASHINDANO YA CAF


 

Samuel Etoo amesema Mataifa yenye Nguvu kisoka ngazi ya Vilabu kama Tanzania yanapaswa kuwa na timu 4 Kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCĆ).


Rais huyo wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT), amesema hayo wakati akizungumza kupitia Mahojiano na Kituo cha Televisheni cha RTI 1.


"Nafikiri ni wakati sahihi kubadilisha mfumo wetu wa upatikanaji wa vilabu katika Mashindano yetu ya #CAFCL na #CAFCC..


"Tunapaswa kufanya kama wanavyofanya watu wa Ulaya na Asia, Mataifa yenye Ligi zenye nguvu hayapaswi kutoa Timu sawa na Mataifa yenye Ligi dhaifu"


"Mataifa kama Tanzania, Afrika Kusini, Congo DR, Senegal, Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Libya kwasababu wanaligi bora wanapaswa kutoa Timu Nne CAFCL na nyengine nne CAFCC.


"Endapo tutatumia mfumo huu utasaidia kuleta ushindani zaidi lakini pia kuongezeka kwa mashabiki wanaofuatilia Mashindano haya.


"Kila bara kwasasa duniani linapambana kuongeza ushindani katika mashindano yao ya Vilabu na sisi Afrika tunatakiwa tubadilike kwasababu binafsi naamini sisi Waafrika ni Bora kisoka Duniani kuliko bara Lolote lile," amesema Etto.

_________

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI