NMB YASHIRIKI MKUTANO MKUBWA WA MADINI DUNIANI

 


 

Benki ya NMB inashiriki katika mkutano mkubwa wa madini duniani, Africa Down Under, Perth, Australia unaomalizika leo.


Mkutano huu wa siku tatu unawakutanisha wadau wa sekta ya madini kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwemo viongozi wa serikali, makampuni ya uchimbaji, wawekezaji na wadau wengine kujadili fursa zilizopo, sera na hali ya jumla ya sekta hiyo barani Afrika.


Mwaka huu, ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ambaye aliwasilisha mada kwa washiriki kuhusu utayari wa Tanzania kushirikiana na wadau wa Australia na mataifa mengine ili kuendeleza sekta hii inayochangia zaidi ya 9% katika pato la Taifa. 


Katika mkutano huu pia, Waziri Mavunde, alieambatana na Balozi wa Tanzania nchini Australia na Japan, Mhe. Baraka Luvanda, alitembelea banda letu na kupokelewa na Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha, ambaye alimfahamisha Mheshimiwa Waziri kuhusu jitihada za benki katika kutoa masuluhisho mahsusi ya kifedha kwa wadau wa sekta ya madini ili kuongeza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi. 


Waziri Mavunde amepongeza juhudi za Benki ya NMB katika kuimarisha sekta ya madini na kuwainua wadau katika mnyororo mzima wa sekta hii, huku akihimiza kuendeleza juhudi hizo hasa kwa wachimbaji wadogo na wa kati.


“Napongeza ushiriki wa Benki ya NMB katika mkutano huu mkubwa wa madini kati ya Australia na Afrika. NMB imetoa mikopo kwenye utekelezaji wa miradi hii kwa baadhi ya kampuni za Australia. Hii ni hatua nzuri ya kukuza sekta ya madini kupitia mchango wa taasisi za fedha,” amesema Mhe. Mavunde.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

ASKOFU CHANDE AISHUKURU SERIKALI KULIPATIA USAJILI WA KUDUMU KANISA LA KARMELI

"WANAUME WAPO GEREZANI, KABURINI"

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI