TAKUKURU DODOMA YAWAASA WANANCHI KUACHA KUWASHAWISHI WAGOMBEA KUTOA RUSHWA

Mkuu wa Taaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Victor Swela amewaasa wananchi kuacha tabia ya kuwashawishi wagombea kutoa rushwa wanaokwenda kujinadi kwao kupata nafasi ya kuchaguliwa.


Amesema kuwa viongozi wanaopatikana kwa rushwa hawatimizi wajibu wao vizuri wa kuwaletetea maendeleo wananchi katika eneo husika.


"Kwanza kabisa ni kupata viongozi wasio na sif na hakubaliki na wananchi katika sehemu husika, na wakati huohuo anajiangalia yeye binafsi kimaslahi badala ya maendeleo ya wananchi,"amesema Swela.


Ametaja athari nyingine kuwa viongozi kama hao mara nyingi hujipendelea kwa kuangalia zaidi maendeleo yao binafsi badala ya wananchi, jambo ambalo linasababisha miradi mingi ya maendeleo kudorora.


Aidha, amewaasa wananchi kuacha tabia ya kutoa taarifa potofu wanapobaini katika eneo fulani kuna viashiria vya rushwa, bali wanachotakiwa ni kutoa taarifa sahihi ili waweze kuchukua hatua zinazostahili.



Swela, ameyasema hayo hivikaribuni wakati wa kikao kuelezea umuhimu wa wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi na wajibu wao wa kukemea vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.


Wakati huo huo akifungua kikao kilichohudhuriwa na viongozi wa dini, taasisi za umma, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla na kufanyika kwenye ukumi wa Cathedral jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu wa Taifa na kuungana kukekemea vitendo vya rushwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Mkuu wa Taaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Victor Swela akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu wa Taifa na kuungana kukekemea vitendo vya rushwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Sehemu ya wananchi wa kada tofauti wakishiriki katika kikao hicho.

Viongozi wa Taasisi, Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara na viongozi wa vyama vya Wafanyakazi katik Mkoa wa Dodoma wakielezewa wajibu wao wa kuzuia rushwa kwenye chaguzi.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI