Mama Lishe wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Februari 4, 2025, tayari kuongoza maadhimisho ya miaka 48 ya CCM kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodfoma kesho. CCM Itatumia maadhimisho hayo kuwatambulisha kwa wana CCM wagombea wao urais kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu ujao. Samia atagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hussein Ali Mwinyi atagombea urais wa Zanzibar na Dkt. Emmanuel Nchimbi atakuwa mgombea mwenza urais wa Tanzania.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments