SPIKA TULIA AFANYA ZIARA OFISI YA KUDUMU YA TANZANIA UN

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, tarehe 11 Februari 2025, amefanya ziara katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), zilizopo Jijini New York, Marekani.


Katika ziara hiyo, Dkt. Tulia amepokewa rasmi na Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman. Ziara hii ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kushirikiana katika masuala ya kimataifa yanayohusu Tanzania ndani ya Umoja wa Mataifa.


Aidha, katika nafasi yake kama Rais wa IPU, Dkt. Tulia anatarajiwa kuongoza Kikao cha Maandalizi cha Mkutano wa 6 wa Maspika Duniani, unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2025 mjini Geneva, Uswisi.


Vilevile, Dkt. Tulia atakuwa Mwenyekiti Mwenza wa IPU-UN Parliamentary Hearing, Mkutano muhimu unaoangazia ushirikiano kati ya Mabunge na Umoja wa Mataifa katika masuala ya maendeleo na utawala bora. Mikutano hiyo miwili itafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Februari 2025, katika Kumbi za Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO

HUYU NDIYE DKT. NCHIMBI, MAKAMU WA RAIS AJAE