Mwenyekiti wa Bunge, ambaye ni Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika akiongoza Mkutano wa 19, Kikao cha 50 cha Bunge jijini Dodoma Juni 20, 2025.
Katika kikao hicho ameongoza mjadala wa kulitaka Bunge kukubali na kupkea na kupitisha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha wa 2025/2026.
Mwanyika akiondoka baada ya kuahirisha bunge hadi Jumatatu Juni 23, 2025. Bunge la 12 linatarajiwa kuhitimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Juni Ijumaa Juni 27, 2025.
Comments