SIMBACHAWENE AVUTIWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Dodoma, Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ametembelea banda la Benki ya NMB katika ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika Jijini Dodoma.


Katika ziara hiyo, Mhe. Simbachawene alipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa taasisi za umma, ikiwa ni sehemu ya mchango wa NMB katika kuboresha huduma za kifedha na maendeleo ya kiuchumi nchini.


Maadhimisho ya mwaka huu yamewaleta pamoja Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Taasisi mbalimbali za Umma, ambapo wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa majukumu yao, sambamba na kuonesha huduma na bidhaa zinazotolewa kwa manufaa ya umma.


Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Juni na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango muhimu wa watumishi wa umma katika maendeleo ya nchi zao na bara kwa ujumla.


Benki ya NMB imekuwa mshiriki hai katika maadhimisho haya kwa kutoa elimu ya kifedha na kuonesha masuluhisho mbalimbali ya kidijitali yanayolenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa Watanzania. 

Waziri Simbachawene akiwa banda la NMB.
Baadhi ya wateja wakipata huduma kwenye banda la NMB.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

NMB YATOA MSAADA WA SH. MILI. 125 KUBORESHA MIUNDOMBINI KATIKA SHULE 15 ARUSHA

ASHUKURU MAFUNZO YA KILIMO JKT YAMEMLIPIA ADA CHUO KIKUU

DKT. NCHIMBI AKIFUATILIA BAJETI KUU YA SERIKALI