Mwanamke nisikilize, wanaume wengi watakutafuta na kukutongoza ukiwa ndani ya ndoa. Unajua kwa nini? Sio kwa sababu wewe ni mzuri sana au wanakupenda sana bali ni kwa sababu wanajua huwezi kuwabana sana na hawatoingia gharama sana kwa kuwa upo kwenye ndoa na unabanwa na majukumu ya familia na kwa asilimia kubwa mumeo ndiye anayekugharamia kukupendezesha wao wanajichapia tu nyama ilale.
Siku ukiachika kwenye ndoa yako, na hao wanaume wote uliokuwa unawaona ni bora kuliko mumeo nao wanakukimbia hawakutaki tena, wanaenda kumhadaa mwanamke mwingine aliyeko kwenye ndoa.
Mwanamke ilinde ndoa yako kwa wivu mkubwa, hata kama mumeo ana mapungufu (yanayovumilika lakini) ukae ukijua kuwa hakuna mwanaume anayekupenda huko nje.
Mwanamke fahamu kuwa mwanaume yeyote aliyeoa akikuambia anakupenda ujue anamaanisha anahitaji ngono tu kisha arudi kwa mke wake japo moyoni akiwa na hatia ya dhambi ya usaliti. Hakupendi anahitaji tu kukata kiu yake ya tamaa ya ngono. Jishikamanishe na mumeo.
Nasisitiza tena mwanamke linda ndoa yako kwa wivu mkubwa, ndoa yako imebeba heshima yako, imebeba sitara yako, imebeba hatma nyingi za watoto wako. Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Credit to Remmy Cameroon
Comments