SERIKALI KUTAFUTA SH. BIL. 4.6 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI KIFANYA NJOMBE

Serikali kupitia Wizara ya Maji imemuahidi Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika kupeleka sh. mil. 200 za kukamilisha ujeni wa mradi wa Maji wa Igongwi jimboni humo. Pamoja na Mambo mengine, ahadi hiyo imetolewa bungeni Mei 12, 2024 na Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew wakati wa kipindi cha maswali na majibu. Awali Mwanyika aliihoji serikali kwamba lini itaanza ujenzi wa mradi wa maji kwenye Mji Mdogo wa Kifanya katika Kata ya Kifanya. Na kujibiwa kama ifutavyo; Mheshimiwa Spika, Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini unakamilika ili kuweza kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wake. Mradi wa maji kwa ajili ya kuhudumia miji Mji Mdogo wa Kifanya uliopo Wilaya ya Njombe umefanyiwa usanifu na kukamilika. Miongoni mwa kazi zinazotarajiwa kutekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na Ujenzi wa kidakio (intake), ujenzi wa tanki la chini (sump well) ujazo wa lita 100,000 pamoja na tanki la kuhifadhia maji lita 300,000 na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji vitano (5). Mradi unalenga kunufaisha zaidi ya wakazi 5484 waishio kwenye Mji Mdogo wa Kifanya uliopo katika Wilaya ya Njombe mkoani Njombe. Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza utekelezaji wa mradi huo unaotarajia kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4,638,708,752.59.

Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika

Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew

 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI