MWENYEKITI UWT MKOA WA PWANI ATUA KIBAHA MJI APANIA KULETA MAGEUZI YA KIUCHUMI KWA WANAWAKE

Na Victor Masangu,Kibaha

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amewahimiza wanawake kuweka misingi imara  ya kutumia fursa za mikopo   ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Hamashauri kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Vullu ameyabainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo ameweza kutembelea katiika  kata mbili  za Tumbi pamoja na Kata ya Kongowe ambapo ameambatana na kamati  ya utekelezaji ya Mkoa pamoja na vingozi ngazi ya Wilaya.
 Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo ameweza kupata fursa ya kutembelea baadhi ya miradi ikiwemo katika sekta ya elimu ambapo ameweza kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa choo salama katika wa sekondari ya  Kibaha pamoja na kituo cha afya Kongowe.

Mwenyekiti  huyo amesema kwamba lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwa ajili ya kuwashukuru umoja wa wanawake UWT kwa kuweza kuwa pamoja na mshikamano wa kukiwezesha chama cha mapinduzi kuweza kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwapoitisha viongozi katika ngazi mbali mbali ikiwemo udiwani, Ubunge  pamoja na nafasi ya Urais.
Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjni Cesilian Ndaru amesema kwamba  lengo lako kubwa  ni kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya kuwa na vitega uchumi ambavyo vutaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kijikwamua kiuchumi.
Katibu Ndaru amebainisha  kwamba umoja huo wameweka mipango madhubuti ya kuwa na miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuanzisha miradii ya kuwa na nyumba za makatibu kila kata kwa ajili ya kuwawezesha makatibu kuwa na sehemu na makazi ya kusihi ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Naye mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Mama Selina Koka ambaye pia ni mke wa Mbunge wa  Jimbo la Kibaha mjini amesema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wanawake katika kuhakikisha kwamba wanaimarisha jumuiya hiyo.

Mama Koka amebainisha kwamba lengo lake  kubwa ni kuendelea kushirikiana kwa  pamoja na viongozi wenzake katika kufanya kazi kwa bidii na kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta chanchu ya maendfeleo ikiwa pamoja na kuwainua kiuchumi wanawake wenzake.
 
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani  imefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo ameweza kupata fursa ya kutembnelea baadhi ya mikradi ya maendeleo ikiwemo katika shule ya sekondari ya wasichana Kibaha pamoja na kituo cha afya Kongowe ikiwa pamoja na kuzungumza na wanawake wa umoja huo.

 






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI