PICHA ILIYOBAMBA ZIARA YA RAIS WA NAMIBIA WILAYANI KONGWA

Mzee mkazi wa Wilaya ya Kongwa akiwa na hamu ya kumuona Rais wa Namibia Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah alipowasili katika iliyokuwa Kambi ya Wapigania Ukombozi Afrika lililopo wilayani humo.

Mzee huyo ambaye alikataa kutaja jina na umri wake anadai alikuwepo wakati kambi hiyo ikifanya kazi na walifurahia maisha waliyokuwa wakiishi na wapiganaji kutoka Namibia, Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe.

Tukio hilo lilijiri wakati wa ziara ya kiongozi huo ambaye pia alitembelea bweni alilokuwa anaishi Rais wa Kwanza wa Namibia, Sam Nujoma, aliweka mashada ya maua kwenye makaburi ya wapigania ukombozi wa Namibia na kiwanja cha kujenga ubalozi wa nchi hiyo nchini katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI