TAIFA STARS YAAGWA KWENDA CHAD

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (kushoto), akimkabidhi nahodha wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Henry Joseph, Bendera ya Taifa, katika hafla ya kuiaga timu hiyo, Dar es Salaam usiku.Inaondoka leo kwenda Chad kucheza na timu ya Taifa ya huko katika michuano ya kuwania kushiriki Kombe la Dunia 2014. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jan Poulsen. (PICHA NA KAMANDA MWAIKENDA)
Bendi ya Kalunde ikitumbuiza katika hafla hiyo.



Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen, akiahidi kuwa timu hiyo itafanya kweli Chad
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, akibofya kitufe kwenye kompyuta, ikiwa ni ishara ya kuzindua tangazo la kampeni ya 'Pamoja Tutashinda' juzi jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuiaga timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), inayondoka leo kwenda Chad kucheza na timu ya Taifa ya huko katika michuano ya kuwania kushiriki Kombe la Dunia 2014. Kulia ni Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa na Kocha wao Jan Poulsen (kulia) katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti inayodhamini timu hiyo.
Wasanii wa kikundi cha Mama Afrika, kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Juma Pinto baada ya kutoa salamu kwa Taifa Stars. Kutoka kulia ni Teddy Mapunda wa SBL, Mjumbe wa BMT,Alex Mgongolwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA