Airtel yakabidhi milioni 50 kwa mshindi wa pili wa MZUKA promo
• Mshindi wa promo ya mwisho MZUKA kupatikana mwanzoni mwa Machi
• Promsheni mpya ya NANI MKALI itaendelea kufaidisha watea na
zaidi ya milioni 200.
Dar es Salaam 22/02/2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imekabidhi kitita cha shilingi milioni 50 kwa mshindi wake wa pili wa
promosheni yao kubwa ya MZUKA inayokaribia kuisha mwishoni mwa mwezi
huu
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema promosheni hii ni ya muda wa miezi mitatu na tuliahidi
kutoa zawadi zenye thamani ya thamani ya hadi milioni 600/= kwa hiyo
leo milioni hizi 50 zinazoenda kwa Bi Khadija Omari Issa Mkazi wa Dar
es Salaam eneo la Magomeni
Kitita hicho cha Airtel MZUKA shilingi milioni 50 tayari kimewekwa
katika akaunti yake na sasa anaweza kuzitumia kuanza kufanikisha
mipango na malengo yake aliyojiwekea
Pia kwa kupitia Promosheni hii ya MZUKA wa Airtel tayari tumesha toa
zawadi nyingine nyingi ikiwemo simu za Sumsung za kisasa zianzotumia
laini mbili zaidi ya 1,200 pia Sumsung Galaxy S2 zaidi ya 360 na vile
vile Sumsung Galaxy 7.0 zaidi ya 180 kwa wateja wetu mbalimbali
walioko nchini Tanzania
Bado mteja wa Airtel unanafasi ya kujishindia zawadi zilizobaki
kupitia promosheni ya mzuka ikiwemo zawadi kubwa ya shilingi milioni
50 ambapo itatolewa kwa mteja mmoja tarehe 2 marchi 2012. Pia bado
zawadi nyingine za simu za Sumsung galaxy kila siku na kila wiki
zinaendelea kutoka kama kawaida
Ili mteja aweze kushinda ni rahisi na pia ni bure. Shiriki kwa kutuma
neno MZUKA kwenda 15565 na namba yako itakuwa inaingia kwenye droo
bure
Nae mshindi wa pili wa promosheni Bi Khadija Omari alisema “Naishukuru
sana Airtel kwa kuniwezesha kujipatia mamilioni haya ya fedha ambayo
msaada mkubwa sana kwangu ninawashauri wenzangu ambao hamjashinda
endeleeni kushiriki kwani mnaweza kuibuka washindi wa ili droo ya
mwisho inayofuata
“Nitaitumia zawadi yangu kuboresha maisha yangu ili niweze kutimiza
ndoto zangu nilizokuwa nazo tangu awali alimaliza kwa kusema Bi
Khadija
Artel Tanzania inaendesha na promosheni nyingine mpya ya NANI MKALI
ambapo zaidi ya milioni 200 zinashindaniwa, Ili kushiriki promosheni
hiyo mteja anatakiwa kutuma nene MKALI kwenda 15656 bure na kisha
ataanza kupokea maswali tofauti na kila atakapokuwa akijibu maswali
hayo kwa kujibu sms hizo atapata pointi na kujiongezea nafasi ya
kushinda.
Kila SMS itatozwa shilingi 350 tu hii ni pamoja na kodi. Promosheni
zote za Airtel zinadhamira ya kuwazawadia wateja wote wa Airtel ambao
wamekuwa wateja wazuri na kutumia huduma za Airtel kila siku.
mwisho
Comments