WANAHABARI WASHINDANA KUONJA BIA TBL

Mtangazaji wa Redio ya Clouds FM, Alex Lwambano akitofautisha rangi za bia kwa kuangalia wakati wa mashindano ya kuonja ladha ya bia yaliyoandaliwa na Ka mpuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Makao Makuu ya TBL mwishoni mwa wiki. Walioibuka washindi katika kinyang'anyiro hicho ni; Mpigapicha wa gazeti la Tanzania Daima, Francis Dande (nafasi ya kwanza), Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori (nafasi ya pili) na Clifod Ndimbo wa Radio Times FM aliyeambulia nafasi ya tatu.

Washindi wa uonjaji wa ladha ya bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa na kukabidhiwa zawadi zao katika mashindano yaliyowashirikisha waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam. Katikati ni Mshindi wa kwanza, Mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Francis Dande, Kulia ni mshindi wa pili Venance Nestory Mpiga picha wa gazeti la Mwananchi na Clifod Ndimbo wa Radio Times FM aliyeambulia nafasi ya tatu.
Mwandishi wa habari wa gazeti la The African, Sylvester Joseph akitofautisha rangi za bia kwa kuangalia wakati wa mashindano ya kuonja ladha ya bia yaliyoandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Makao Makuu ya TBL, mwishoni mwa wiki.



Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni mbili za bia, Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano ya kuonja bia
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni tatu za bia, Mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Francis Dande ambaye aliibuka mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuonja bia yaliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori (nafasi ya pili) na Clifod Ndimbo wa Radio Times FM aliyeambulia nafasi ya tatu.
Mtaalamu wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Deusdedith Maganga (kushoto), akitoa maelezo kwa waandishi wa Mkoa wa Dar es Salaam, jinsi unga wa mahindi unavyotumika kutengenezea bia walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Deusdedith Maganga (kulia), kuhusu hatua mbalimbali za utengenezaji wa bia walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni moja ya bia, Mtangazaji wa Radio Times FM, pigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano ya kuonja bia yaliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.