NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE
Alhamdulillah ala kulli hal Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima. UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini. Ninawaomba wanakimji wen...
Comments