Whitney Houston afariki hotelini

LOS ANGELES, Marekani

ALIYEKUWA nguli na malkia wa muziki wa Pop duniani, Whitney Houston amekutwa amefariki dunia kwenye hoteli aliyokuwa amefikia mjini Los Angeles, Marekani.

Whitney alikutwa amefariki dunia kwenye chumba cha Hoteli ya Beverly Hilton aliyokuwa amefikia ambako alikwenda kwa ajili ya kuhudhuria hafla kabla ya kuanza kwa sherehe za tuzo za muziki za Grammy.

Whitney aliyetamba kwa nyimbo zake zake nyingi za masuala ya mapenzi kama vile 'I Will Always Love You', pia alitamba kwenye anga ya filamu kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.

Kipaji chake cha muziki kiliharibiwa na matumizi ya dawa za kulevya zilizosababisha kuharibika kwa maisha yake na baadaye kuvunjika kwa ndoa yake iliyokuwa imejaa matatizo mengi na mumewe, Bobby Brown mwaka 2007. Whitney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.

Whitney na wapambe wake walichukua karibuni vyumba vyote vya ghorofa ya nne ya hoteli hiyo na walikuwa wakiponda starehe tangu Alhamisi.

Whitney ambaye aliuza zaidi ya nakala milioni 55 za nyimbo zake nchini Marekani pekee, alikutwa amefariki kwenye chumba chake hotelini na juhudi za madaktari kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.

Mwili wake ulihamishwa mochari kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa sababu ya kifo chake ingawa polisi wanasema hadi sasa hakuna dalili ya kufanyika kwa faulo yoyote katika kifo chake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*