Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Mkuu wa Majeshi mstaafu, marehemu Jenerali Ernest Mwita Kiaro wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Tarime, mkoani MaraAmiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Mkuu wa Majeshi Mstaafu Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kiaro wakati wa mazishi yake huko Tarime,mkoani mara jana(picha na Freddy Maro).
CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO
Chama cha Kulinda na Kuwatetea Walimu Tanzania (CHAKUWAHATA) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata la baadhi ya wakurugenzi kukiuka sheria ya kuwaruhusu walimu kujiunga na chama hicho hivyo makato ya fedha za mishahara yao kuingizwa kwenye chama hicho. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Herman alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wao unaofanyika jijini Dodoma. Walimu ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kupitia upya rasimu ya katiba ili ieendane na wakati.
Comments