PROFESA LIPUMBA AZUIWA KUMJULIA HALI DK ULIMBOKA

 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye leo jioni alikwenda Muhimbili kwa nia ya kumjulia halia, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stevene Ulimboka, amezuiwa kumuona.

Profesa Lipumba, ambaye alikuwa na nia nzuri ya kumjulia hali daktari huyo, alizuiwa na madaktari wenzie kwa madai kwamba hawamruhusu mtu yeyote kwani Dk. Ulimboka alikuwa anaendelea na matibabu ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ICU.

Alipofika hospitalini hapo, kwanza alikwenda kwa Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Jumaa Almas ambaye pia alimueleza hivyo. Profesa Lipumba ni kiongozi wa kwanza wa kisiasa kwenda Muhimbili kutaka kumjulia hali Dk. Ulimboka.
                                                DK Ulimboka akiwa katika chumba hicho cha icu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

YANGA BADO POINTI 2 TU ITANGAZE UBINGWA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA