HOT NEWS: MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi AHUKUMIWA kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God
of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani
kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali
wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa
Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya
Daniel Mwasumbi
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God
of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe
akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30
Jela
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God
of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka
Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God
of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na
waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
Waumini Mbalimbali
wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30 |
Binti anaye daiwa
kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of
Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha
miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa
mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya
Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi
uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo
Neema Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo
kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na
Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa
Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito
kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa
akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu
cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles
Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda
kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka
19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na
maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali
ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya
Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha
malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa
adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa
watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa
hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu
kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika
kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo
zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania
kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika
Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama
yake.
Habari ,Picha na Mbeya yetu Blog
Comments