VIDEO!!!! TAZAMA TUKIO ZIMA KUTOKA MAHAKAMANI SAKATA LA BABU SEYA NA MWANAYE KIFUNGO CHA MAISHA....ITAZAME HAPA INASIKITISHAAA!!!
Mahakama ya rufaa imetupilia mbali ombi la kupitia upya hukumu ya Babu Seya na Mwanaye.
Kwa mara nyingine harakati zao za
kujitoa katika adhabu hiyo zimegonga mwamba baada ya mahakama ya rufani
kupigilia msumari wa mwisho uliozima harakati zao za kujinasua katika
adhabu hiyo, baada ya kutupilia mbali maombi yao ya marejeo ya hukumu ya
rufaa yake.
Akisoma maamauzi hayo naibu msajili Mh
Zahra Maruma amesema mahakama imejiridhisha kuwa hakuna jambo jipya wala
la msingi katika maelezo yaliyotolewa na upande wa walalamikaji.
Akaongeza kuwa mambo mengi ambayo
wamesema mahakamania hapo ni yale yale ambayo waliyasema walipokuwa
wamekata rufaa na hivyo mahakama imeona maamuzi yaliyofikiwa mwanzo ni
busara yabaki jinsi yalivyo uamuzi huo uliibua machungu si tu kwa
wafungwa hao ambao walitoa kauli za kukata tamaa, bali pia kwa wakili
wao Gabriel Mnyele ambaye alitoa kuali kuwa sasa hakuna namna nyingine
ya kuwachomoa katika adhabu hiyo isipokuwa kwa miujiza tu.
Comments