Sehemu
kubwa ya wafanyakazi wa mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia TAZARA
Stesheni ya Mbeya nchini Tanzania, wamegoma kufanya kazi tangu leo
asubuhi.
Mgomo
huo ambao wenyewe wameuita kuwa ni mgomo baridi umesababishwa na mamlaka
hiyo kushindwa kuwalipa mishahara yao kwa miezi mitano sasa.
Kwa
majibu wa mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye yupo safarini kuelekea
Kapiri Mposhi Zambia akitumia train ya TAZARA, mgomo huo umesababishwa
kukwama kwa train hiyo kuendelea na safari yake hadi kufikia jioni hii.
MSIMAMO WAO
Amesema
train ya abiria kutoka Dar es Salaam ilifika mjini Mbeya saa 4.30
asubuhi na hapo wafanyakazi hao waliipokea train hiyo kwa wimbo wa
Solidarity forever.
Wafanyakazi
hao wameiambia BBC kuwa wanailalamikia Serikali ya Tanzania kwa
kuwapuuza madai yao huku serikali ya Zambia ikiwalipa wenzao wa upande
wa pili.
Kwa
muda mrefu TAZARA imekuwa katika kipindi kigumu cha uendeshaji wa
shughuli zake kutokana na kukosa ruzuku ya serikali zote mbili.
Baada
ya mivutano na mikakati ya kuboresha shughuli za kabiashara ya mamlaka
hiyo, iliamuliwa kuwa kila nchi iendeshe train yake na iishie mpakani
kwenye miji midogo ya Tunduma (Tanzania) na Nakonde (Zambia).
TRENI KUISHIA MPAKANI
Mpango
huo ndiyo kwanza umeanza kwa train ya abiria iliyoondoka jana Jumanne
Dar es Salaam na nyingine ikitoka New Kapiri Mposhi na zitakutana
mpakani baadae leo jioni.
Kwa mpango huo wasafiri wanaokwenda upande wa pili wa nchi nyingine watalazimika kushuka na kuingia kwenye train nyingine.
BBC
inafuatilia kuona mchakato wa kuhamisha wasafiri hao utakavyokuwa, kwa
kuzingatia miongoni mwa wanaosafiri kuna watoto, wazee vikongwe,
wajawazito, Lakini pia kunakuwa na walemavu na wenye mizigo mingi.Chanzo
BBC Swahili
Comments