Akilia baada ya kula kichapo.
BALAA! Siku
chache tu baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo
wawili ambao majina yao hayakufahamika haraka wamejikuta wakila kichapo
kutoka kwa mabaunsa kufuatia kuchelewa kutoka ndani ya baa waliyokuwa
wakipombeka. Tukio hilo la aina yake lilijiri Agosti 5, mwaka huu katika baa hiyo mpya iliyopo Sinza ya Afrikasana jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa
kuwa, warembo hao waliambiwa mapema kuwa ifikapo alfajiri wasionekane
kwenye eneo la baa hiyo lakini wao waliendelea kupombeka mpaka jua
linachomoza ndipo mabaunsa walipowaondolea uvivu kwa kuwapa kipigo. Mmoja
wa warembo hao ambaye alionekana kukerwa na kitendo cha mwenzake
kupigwa hadi kutokwa damu aliwalalamikia mabaunsa hao kuwa
hawajawatendea haki kwa kuwafukuza kama mbwa na kipigo juu
Akitokwa na damu juu ya jicho la upande wa kulia baada ya kuchezea kichapo kikali.
Kwa
vile hawakuwa na nguvu za kupigana na mabaunsa hao, warembo hao
waliporomosha matusi ya nguoni na kujaza watu waliokuwa wakienda
makazini asubuhi hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya
mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio, hasa wanaume walisikika wakipongeza
kitendo cha warembo hao kuchezea kichapo wakisema wamezoea kukesha eneo
hilo mpaka kunakucha.
Mashuhuda hao walikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa wanahisi warembo hao wanajihusisha na biashara ya ‘udada poa’.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia mkasa huo.
“He!
Wamezoea hao! Ni sawa mabaunsa wawaoneshe kazi. Watu gani wapo baa hadi
muda huu wa asubuhi kweupe?” alisikika mmoja wa mashuhuda hao.
Kilio kikubwa cha mabaunsa hao
kilikuwa ni kutaka kusimamia heshima ya baa hiyo kwa vile wateja
wanaofika hapo ni wenye heshima zao.
“Msije tena hapa, sisi
hatuwataki muda wa asubuhi wala mchana, tulishasema sana lakini
hamsikii, mnataka kutukimbizia wateja siyo?” alisema mmoja wa mabaunsa
hao.
Wakishauliana jinsi ya kumsaidia mwenzao.
Mwisho
wa sakata hilo, warembo wengine walitafuta usafiri wa Bajaj na kumbeba
mwenzao aliyepigwa sana mpaka kutoka manundu na kuondoka huku
wakiendelea kuvurumisha mitusi kwa mabaunsa hao na kusema wanakwenda
kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar.
Mapaparazi wetu waliifuatilia Bajaj hiyo na kuiona inaelekea maeneo ya Sinza ya Mapambano badala ya polisi.
Baadhi ya wateja wa baa hiyo
walisema wakati wa Mfungo wa Ramadhan, warembo walipungua eneo la baa
hiyo lakini sasa wamerudi tena ambapo sasa wanapatikana kuanzia saa moja
jioni hadi jua linapochomoza kesho yake
Comments