DIWANI LTP LUPINGU AZIDI KUFUNGUKA ADAI ATAENDELEA KUFANYA KAZI NA MBUNGE WA CCM ,AWASHANGAA WAPINZANI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
Diwani wa kata ya Lupingu John Kiowi (TLP) kushoto akifurahia kauli ya mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) ya kumtaka kuhamia CCM ili kuendelea kufanya kazi pamoja |
Wananchi
wa kijiji cha Ntumbati kata ya Lupingu wakishirikiana na mbunge wa
jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto ) kubeba nguzo za umeme.Soma zaidi |
Viongozi mbali mbali wakishiruikiana na mbunge pamoja na wananchi kusimika nguzo ya umeme |
mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana na wananchi wake na viongozi wa CCM kata ya Lupingu kusimika nguzo za umeme kwenda kijiji cha Ntumbati |
Mbunge Filikunjombe na wananchi wakifukia nguzo ya umeme |
Mbunge Filikunjombe na wananchi wakishiriki kufyeka miti kwa ajili ya kupata njia ya kupiga nguzo za umeme kwenda kijiji cha Ntumbati |
Wanawake wakiwa na watoto mgongoni wakijitolea kushiriki maendeleo |
Mbunge Filikunjombe akiwapongeza wanawake wa kijiji cha Ntumbati ambao walijumuika na waume zao katika kushiriki maendeleo ya kufyeka miti ili kupata njia ya kupita umeme huku waume zao wakichimba mashimo na kubeba nguzo |
Filikunjombe akiwa na chombo chenye chakula ambacho walimletea wananchi hao ili baada ya kazi aweze kula |
Wanawake wa kijiji cha Ntumbati wakiendelea kufyeka miti |
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (mwenye shati la kijani)na timu yake wakiongoka baada ya kumaliza siku ya kwanza ya kuchimba mashimo na kubeba nguzo |
Na matukiodaima.co.tz
WAKATI uchaguzi mkuu mwaka 2015 ukinukia diwani wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe John Kiowi amesema
kuwa hana sababu ya kuendelea msimamo wake wa kukumbatia itikadi za
chama chake na badala yake ataendelea kumuunga mkono mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe( CCM)katika kuwaletea wananchi maendeleo.
”
ndugu zangu wananchi kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge wetu
mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe pia amekuwa mstali wa mbele
katika kushiriki tofauti na wana siasa wengine ambao muda wote wao
ni watu wa majukwaani ila vitendo sifuri …..nasema Ludewa imempata
mbunge na niweke wazi hapa mimi sio mpinzani mbabaishaji kama
walivyo wengine ambao kila kukicha wao wanawaza kuipinga serikali na
maandamano badala ya kuandamana kama hivi kuja kushirikiana na na
wananchi kuleta maendeleo ...."
Kauli ya diwani huyo
ilikuja baada ya mbunge Filikunjombe na wananchi wake kumtaka
kurejea CCM ili aweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi kuwatumikia vema
wananchi wake kwa kuwa ndani ya CCM.
Akizungumza wakati wa
kumkaribisha mbunge Filikunjombe kushiriki shughuli za maendeleo ya
kuchimba mashimo ya nguzo za umeme na kusimika nguzo za umeme kutoka
kijiji cha Nindi kwenda kijiji cha Ntumbati kata ya Lupingu ,diwani
Kiowi alisema kuwa kati ya wabunge wa CCM ambao anawakubali na yupo
tayari kufanya nao kazi na kusikiliza ushauri wao ni pamoja na
Filikunjombe.
" Mheshimiwa mbunge kwanza nataka
kukuhakikishia kuwa ni mara chache sana kuna diwani wa upinzani
akifanya kazi na mbunge wa CCM kama njia ya kutekeleza ilani ya CCM
......kwani sisi wapinzani ni watu wa kupinga kila jambo hata kama
linamanufaa kwetu wenyewe lakini nakuhakikishia mimi kama diwani wa
TLP hapa kata ya Lupingu natamka wazi kwanza nitawakamata na
kuwachukulia hatua wale wote wanaopinga maendeleo makubwa ambayo
unatuletea kata ya Lupingu bila kujali ni kata ya upinzani.....ila
na mimi nitamke wazi kuwa napenda sana kufanya kazi na wewe" alisema
diwani huyo bila kusema kama yupo tayari kurejea CCM ama lah.
Kwani alisema uchapakazi wa mbunge
huyo unawavuta wengi hata ambao si wananchi wa jimbo la Ludewa leo
wanapenda utendaji kazi wake hivyo kwa mwana Ludewa ambae hatataka
kuonyesha ushirikiano basi ana lake jambo ila kati ya wapinzani
ambao wanatambua mchango mkubwa wa maendeleo unaofanywa na mbunge
huyo ni pamoja na yeye .
Alisema kwa kata hiyo ya Lupingu
toka utawala wa Filikunjombe umeanza mwaka 2010 kumekuwepo na mafanikio
makubwa ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na wananchi hao kuanza
kupata usafiri wa uhakika tofauti na awali ambapo walikuwa
wakilazimika kutembea kwa miguu na mizigo kichwani kwa zaidi ya
kilometa 50 hadi Ludewa mjini.
" Leo wananchi wa Lupingu ambao
tulikuwa tukilia kuwa serikali imetutelekeza na wakati mwingine
kuhisi kama tupo nchi ya Malawi leo hii barabara nzuri imejengwa
,umeme wa uhakika unaletwa sasa Mungu atupatie nini zaidi ya
Filikunjombe ......nasema wananchi wangu tumehangaika sana kutafuta
mbunge Ludewa na kila baada ya miaka mitano tulikuwa tukichagua
mbunge mwingine ila kwa huyo wa sasa tunasema hatuhitaji mtu mwingine
tunahitaji maendeleo kama haya"
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe
mbali ya kuwapongeza wananchi hao wa kata ya Lupingu kwa kuonyesha
mfano wa kujitolea kuchimba mashimo ya kusimika nguzo za umeme
pamoja na kufyeka miti inayopita katika laini ya umeme bado
alisema wameonyesha uhitaji mkubwa wa umeme na kuwa wananchi wa
pekee nchini ambao wamekubali kufyekewa mazao na miti yao bila
kudai fidia ili umeme upite .
Kuhusu
mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa kwa kasi ambayo
wananchi wanaenda nayo katika kujitolea nguvu zao kuchimba mashimo
na kusogeza nguzo katika mashimo hayo ni wazi mradi huo wa umeme
utakamilika kabla ya Desemba mwaka huu .
Aidha
alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010 ni kijiji kimoja
pekee cha jimbo hilo la Ludewa ambacho kilikuwa na umeme wa mafuta
ila sasa zaidi ya vijiji 10 vina umeme na kuwa hadi sasa jumla ya
vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu
za serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki
Dayosisi ya Njombe.
Alisema iwapo wananchi hao wangekuwa
kama wale wa mijini ama mikoa mingine ambao wamekuwa wakikwamisha
miradi kuanza kwa wakati kutokana na kudai fidia kwa kila kitu basi
yawezekana umeme kufika Lupingu ungechukua muda mrefu zaidi hasa
kutokana na wingi wa miti ,mashamba ya mihogo na mali nyingine ambazo
zingepaswa kufanyiwa tathimini kabla ya kuondolewa .
Kwani alibainisha kuwa haoni sababu ya
yeye kuendelea kuishi mjini wakati wapiga kura wake wana matatizo
chunngu mzima hivyo lazima akipata muda wa mapumziko kukimbia
jimboni kuhamasisha maendeleo na kutekeleza ahadi zake badala ya
kustarehe mjini .
Comments