SOKO LA PARETO NI UHAKIKA WANANCHI KILOLO LIMENI PARETO -DC ASIA



mkuu  wa  wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa Asia Abdalah  wa  tatu  kushoto  akishiriki  kupanda  miche  ya  Pareto  kwenye  shamba  la mtaalam  wa  Pareto Kilolo wakati wa  uzinduzi  wa kilimo  cha Pareto leo

DC  Kilolo katikati  akipata  maelezo ya miche ya Pareto 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo na  timu ya uhamasishaji wa kilimo  cha Pareto  wakitoka  kutazama  vitalu  vya miche ya  Pareto 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia  Abdalah  akitazama  vitalu  vya  miche  ya  Pareto  miche ambayo inatolewa  bure kwa  wakulima 
Mtaalam  wa  kiwanda  cha  Pareto Mafinga Godfrey  Mbeyela  kulia  akishirikiana na  Dc Kilolo  Asia Abdalah kupanda Pareto
Na MatukiodaimaBlog

MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ameanza jitihada za kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulima zao la Pareto kama zao la biashara.

Akizungumza na wananchi wa Udekwa na Lulanzi leo, amesema kuwa Kampeni maalum ya kuhamasisha kilimo cha zao La Pareto zimeanza leo  kwa kupanda Pareto pia kuona vitalu vya miche ya pareto.

Alisema kimsingi miche hiyo itatolewa bure kwa kila Mwananchi anayehitaji kulima zao hilo.

Alisema pamoja na kupanda mazao mengine ya Chakula na biashara wasiache kupanda japo hekari moja ya zao La Pareto.

Mkuu huyo alisema kuwa  zoezi La uhamasishaji upya wa zao La Pareto litafanyika katikati kata mbali mbali za Wilaya ya Kilolo.

Kwani kati ya Wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao La Pareto kwa mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao hilo.

Kuhusu soko aliwataka wakulima kuondoa hofu kwani soko kwa sasa ni uhakika

"Nawaagiza mabwana shamba kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kuwapa Elimu juu ya kilimo cha Pareto"

Alisema kuwa zao La pareto limekubali sana Wilaya ya Kilolo kutokana na hali ya hewa ya ubaridi na kuwa zao hilo halihitaji mbolea

Aidha aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi vya kulima zao hilo japo mtu mmoja mmoja anaruhusiwa kulima

"Mimi mwenyewe nitatafuta eneo La kulima Pareto… ila sisemi muache kulima mahindi kwenye heka zako 10  tenga heka moja ya Pareto"

Katika hatua nyingine amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mbegu za muda mfupi zaidi.

Mtaalamu wa Kiwanda cha Pareto Mafinga Godfrey Mbeyela alisema kwa mbegu za Pareto zimeandaliwa na wanategemea wananchi zaidi ya 40 elfu kulima zao hilo.

Alisema kwa wilaya ya Kilolo daraja La chini litanunuliwa kwa Tsh 2000 Kwa wakulima wa Pareto Kilolo

Alisema kuwa soko la Pareto liliyumba kutokana na mwekezaji aliyekuwepo ila sasa soko lipo La uhakika na kuwa pesa zitalipwa kijijini moja kwa moja.

Alisema kuwa kuwa katika Wilaya nyingine kama Ludewa na Njombe  wanagombea kulima zao hilo.

Hivyo aliwaomba viongozi   wa dini mbali mbali kutumia Nyumba za ibada kuhamasisha wananchi kulima zao hilo.

Kwa  upande  wao  wananchi  wa Kilolo  wameeleza  kufurahishwa na utaratibu  huo  wa Kiwanda  kugawa  miche  bure na  kuwa  wapo tayari  kuanza  tena  kulima  zao  hilo ambalo awali  walikuwa  wakilima kwa  wingi  zaidi 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU