KIJAICOS YAUNDA KAMATI KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI

 Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika  cha Akiba na Uwekezaji -SAICOS (KIJAICOS), Rwihula Daniel (katikati) akiongoza mkutano mkuu wa ushirika huo, leo kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti , Nasra Mohamed na Adam Ngamange ambaye ni Mjumbe wa Bodi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Na Richard Mwaikenda,Ilala

CHAMA cha Ushirika cha Akiba na Uwekezaji (KIJAICOS) kimeunda kamati maalumu ya kutafuta fursa za uwekezaji ili kuuboresha ushirika huo.

Kamati hiyo ya watu sita imeundwa leo wakati wa mkutano Mkuu wa Kijaicos uliofanyika katika Hoteli ya Lamanda, Ilala, Dar es Salaam.

Waliochaguliwa kuunda kamati hiyo ni; Mwenyekiti wa Kijaicos, Rwihula Daniel, Neema Ngowi, Rihard Mwaikenda,Pascal Njereka, Mwalimu Abdallah na Mishomari.

Wametakiwa kufanya utafiti wa miradi inayofaa kwa Kijaicos kuwekeza na kupata faida ili faida inayopatikana wafaidike nayo wanahisa wa Saicos kwa kupata gawio.

Hivi karibuni Kijaicos iliwekeza sh. 362,000 mizinga 10 kwenye mradi nyuki unaoendeshwa na Taasisi ya Maisha Bora Human Development Centre. Hadi sasa mradi huo umeingiza sh. 1,500,000.

Mwenyekiti ameauambia mkutano kuwa Kijaicos iliwekeza pia UTT SH. 500,000 na kupata faida sh. 60,000, Kukamua mafuta ya mchaichai waliwekeza sh. 1,100,000 yaliuzwa mafuta na kupata sh. 900,000 hivyo kuingia hasara ya 200,000.

Mwenyekiti alitaja changamoto zinazoikabili Kijaicos kuwa ni  kukosa watendaji wa kutosha na wenye ujuzi, kukosa fedha za kuwekeza katika miradi mikubwa, kukosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa baadhi ya wanachama.

Mwenyekiti Daniel, aliwasome wanachama taarifa ya fedha ambapo viingilio vya wanachama 73 imefikia sh.3,650,000,  Michango ya Hisa sh. 3,170,000 na malipo ya kila mwezi ni sh.5,505,000. 

Mwenyekiti aliwaomba wanachama kuendele kununua hisa na kuchangia ada za kila mwezi ili kuifanya Kijaicos kuwa hai na kuendelea na mipango mikubwa ya uwekezaji itakayotoa faida kubwa.



 Daniel akifafanua jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia ni wajumbe wa Bodi ya Kijaicos, Stellah Ngulukulu,Sylvester Kapya, Abdalah Mlangwa na Ngamange
Baadhi ya wanachama wakiwa kwenye mkutano
 Wajumbe wakisikiliza kwa makini maendeleo ya mkutano
 Mwanachama wa Kijaicos, Pascal Njereka akichangia hoja
 Mjumbe wa Bodi ya Kijaicos, Adam Ngamange akifafanua baadhi ya hoja
 Mwanachama Hawa Bedui akichangia moja ya hoja za mkutano huo
 Mwanachama wa Kijaicos, Rehema Ally  akichangia hoja wakati wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni wanachama Neema Ngowi, Hawa Bedui.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 0715264202

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI