KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameibuka na kusema kiungo wake, Pacome Zouzoua yupo tayari kuanza kucheza na leo Jumatano kuna uwezekano akampa nafasi, lakini itategemea na mazoezi ya mwisho.
.
Mara ya mwisho Pacome kuonekana uwanjani akiitumikia Yanga ilikuwa Machi 17, mwaka huu walipofungwa mabao 2-1 na Azam katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Mkapa, na siku hiyo aliumia na kutolewa uwanjani.
.
Akizungumzia utayari wa Pacome kucheza mechi ya dhidi ya Tabora United, Gamondi amesema: “Anaweza kuwepo kwa sababu hivi sasa ameanza kufanya mazoezi ya kawaida, tutaangalia katika mazoezi nini kitatokea lakini inawezekana akacheza.”
.
“Kama tusingekuwa na mechi hii (dhidi ya Tabora United), basi uhakika mechi ijayo ya ligi (Mei 5 dhidi ya Mashujaa) angeanza kucheza angalau kwa dakika 30.”
Nene Yanga Fans HQ
Comments