💬Kitu kingine kizuri kuhusu Yanga katika miaka ya karibuni ni namna ambavyo wanaweza kupokea kipigo bila ya kuvurugana. Ni nadra kusikia wanawashutumu wachezaji wao au wanaushutumu uongozi.
Mara nyingi wanapokea kipigo na kwenda kutafakari ofisini bila ya kelele. Kwa namna hii inakuwa rahisi kwao kuibuka katika mechi zijazo na kufanya vema. Ni tofauti na wapinzani wao ambao mara nyingi wamekuwa wakishindwa kuhafiki kipigo au kutoka sare bila ya kutoa shutuma kwa wachezaji au viongozi.
Nadhani Yanga wanakiamini sana kikosi chao kiasi kwamba wanajua wataibuka upya vema ndani ya wiki moja tu. Hili ni jambo zuri kwao. Tazama namna walivyokabili vipigo kutoka Ihefu na wengineo. Walikaa kimya bila ya shutuma kwa wachezaji na hii inawasaidia sana.
—EDO KUMWEMBE
#FutbalPlanetUpdates
Comments