Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ Mkoani Tabora tarehe 21 Disemba 2024.
Nishani alizovisha ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Aidha,Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza na Wanajeshi Kanda ya Magharibi Jenerali Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwatunuku Nishani hizo.
Aidha, amewatakia Heri ya Christmas na Mwaka mpya Wanajeshi wote Nchini huku akiwataka Kuviishi Viapo Vyao walivyoapa, kufanya kazi kwa Nguvu zote kwa Uhodari, Uaminifu, Utii na Nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi, kulinda Katiba na Kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Comments