WANAVIJIJI WAIPOKEA ZAWADI YA MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA SHANGWE TELE




Leo, Kituo cha Afya cha Kata ya Bugwema kimepokea Gari jipya la Wagonjwa (Ambulance) kutoka kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Wanavijiji kutoka Kata hiyo yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji) wamemshukuru sana Mhe Rais wetu kwa kuwapatia gari jipya la wagonjwa (Ambulance).


Wanavijiji hao wameahidi kumpatia Mhe Rais wetu kura zote za Kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani (2025).


*Kuongezeka kwa "Ambulances" Jimboni mwetu:*


(i) Ambulance No. 1

Hii iko kwenye Hospitali ya Halmashauri/Wilaya, Kijijini Suguti


(ii) Ambulance No. 2

Hii iko kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Bugwema, Kijijini Masinono 


Wananchi wa Musoma Vijijini wanamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia "Ambulances" hizi mbili mpya - Ahsante sana!


(iii) Ambulance No. 3

Hii iko kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Murangi, Kijijini Murangi. Mbunge wa Jimbo alipewa Ambulance hii kutoka Serikali ya Japan


(iv) Ambulance No. 4 (gari dogo)

Hii iko kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Mugango, Kijijini Kwibara. Mbunge wa Jimbo alishirikiana na rafiki zake kununua "Ambulance" hii ndogo


(v) Ambulance No. 5 (gari dogo)

Hii iko kwenye Zahanati ya Nyakatende iliyoko Kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu. Mbunge wa Jimbo alishirikiana na rafiki zake kununua "Ambulance" hii ndogo


(vi) Ambulance No. 6 (gari dogo)

Hii iko kwenye Zahanati ya Kurugee, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi. Mbunge wa Jimbo alishirikiana na rafiki zake kununua "Ambulance" hii ndogo


(vii) Ambulance No. 7 (gari dogo)

Hii imehamishwa leo kutoka Kituo cha Afya cha Bugwema kwenda Zahanati ya Rusoli, Kijijini Rusoli. Mbunge wa Jimbo na rafiki zake waliinunua hii "ambulance"


*Uboreshaji wa Huduma za Afya Jimboni mwetu:*


Wanavijiji wanaendelea na ujenzi wa zahanati mpya 17. Baadhi ya hizi zahanati tayari zimeanza kupokea michango ya fedha kutoka Serikalini.


Zahanati zinazotoa huduma: 28

    (24 za Serikali, 4 za Binafsi)


Vituo vya Afya: 6

     (5 vinatoa huduma, 1 kinaanza Jan 2025) 


Hospitali ya Halmashauri/Wilaya: 1

      (inatoa huduma za afya)


*WITO:*

Wana-Musoma Vijijini, rafiki zetu na "wadau wengine" wa maendeleo tuendelee kuchangia ujenzi wa zahanati mpya 17 vijijini mwetu - tunafanikiwa!


Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

Matukio mbalimbali ya upokeaji wa "Ambulance" mpya ya Kituo cha Afya cha Kata ya Bugwema. Hii ilikuwa leo Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema 


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 


P. O. Box 6

Musoma 


Tarehe:

Jumatatu, 23 Dec 2024

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO